
Wakimbia Kijiji baada kushindwa kutoa ufafanuzi wa michango ya…
Afisa Mtendaji na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha KONGO katika kata ya UPUGE,wilaya ya UYUI mkoani TABORA wamekimbia kijijini hapo baada ya kushindwa kutoa ufafanuzi wa michango ya fedha zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara kijijini KONGO,Diwani wa kata ya UPUGE,MUSSA SAFARI amesema kuwa walikubaliana na wanakijiji kukutana ili kuweza kupata ufafanuzi wa mahali zilipo fedha za michango ya shule na fedha za uuzaji wa miti aina ya Mikaratusi.
Nao wananchi wamesema kuwa ni vyema viongozi wa kata ya UPUGE na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wawatafute viongozi waliotoroka na kuhakikisha fedha zao za michango yao zinapatikana.