Wakulima wa tumbaku katika kijiji cha ILALWANSIMBA kata ya…

Wakulima wa tumbaku katika kijiji cha ILALWANSIMBA kata ya ISIKIZYA wilaya ya UYUI wamewaomba wataalamu kutengeneza mabani banifu ya majaribio kukaushi zao hilo ili kufahamu ubora wake.
Hayo yamebainisha na baadhi ya wakulima wa kijiji hicho ambao wamejenga mabani hayo kwa maelekezo ya wataalamu ambayo hajakausha vizuri tumbaku katika msimu wa tumbaku uliopita.
FABANO KIMBAI ni mmoja wa wakulima hao amesema kuwa tumbaku aliyokaushia katika mabani banifu aliyojenga iliharibika.
Hatua hiyo imeungwa mkono na TITO MSALENGE kwa kusema kuwa ni vizuri kama mabani banifu yataboreshwa baada ya kubaini mapungufu yaliyopo ili yawasaidie kutotumia kuni nyingi.

Kwa upande wake CHAUSIKU JAMES amesema iwapo majaribio yatafanyika na kutoa matokeo mazuri watatumia mabani banifu ili kuondokana na kutumia fedha nyingi kununua kuni za kukaushia tumbaku.Wakulima wa tumbaku wamekuwa wakishauriwa kutumia mabani bunifu kukaushia tumbaku ili kutunza mazingira kwa kuepuka kukata miti ambayo hutumika kukaushia zao hilo kwa mabani ya kawaida.