
Wamiliki wa Mabasi, Madereva na Abiria watakiwa kutii kanuni…
Wamiliki wa mabasi,madereva na abiria wametakiwa kutii sheria na kanuni za usafirishaji ili kupunguza kero na kadhia kwa abiria.
Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu – SUMATRA,JOSEPH MICHAEL amesema watu WATATU wamekamatwa kwa kukiuka kanuni ya 23 ya usafirishaji ambayo inakataza kufanya biashara,mahubiri na burudani ndani ya mabasi.
Ameongeza kuwa wakati wote wa safari kwa mujibu wa kanuni ya usafirishaji, mmiliki wa basi ambaye kwa wakati huo ni dereva na kondakta watawajibika iwapo watakiuka kanuni hiyo.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani,Manispaa ya TABORA,IBRAHIM WAZIR I amesema kuwa kuwepo kwa kanuni za usafirishaji kumepunguza vitendo vya wizi kwa sababu baadhi ya wafanyabiashara wanaoingia kwenye mabasi hayo siyo waaminifu.
Kwa mujibu wa kanuni ya 23 ya usafirishaji ya mwaka 2017 kifungu B pia kinaeleza kwamba mtu kufanya biashara,siasa,kuhubiri au kutoa burudani ndani ya magari ya abiria ni kinyume cha kanuni hiyo.
Mwandishi: NAJJATH OMAR, CG FM.