Wananchi mkoani TABORA wameshauriwa kuchunguza afya zao mara kwa…

Wananchi mkoani TABORA wameshauriwa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Ini.
Ushauri huo umetolewa na Daktari NOVATUS NGOLOMA kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa TABORA- KITETE wakati akizungumzia athari zinazotokana na ugonjwa wa homa ya ini.
Daktari NGOLOMA pia amesema jamii inapaswa kuzingatia kanuni bora za usafi, kuepuka ngono zisizo salama na kutumia vema elimu ya afya kwa vijana ili kukabiliana na maradhi hayo.
Shirika la Afya Duniani- WHO limethibitisha kuwa ugonjwa wa homa ya ini ni tishio zaidi hasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na hapa Daktari NGOLOMA anathibitisha kuwa TANZANIA ni miongoni mwa nchi waathirika.
Mapema mwezi Agosti mwaka huu,Mkurugenzi Mtendaji ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa uhalifu na dawa za kulevya, YURY FEDOTOV alisema kuwa ugonjwa wa homa ya ini,Hepatitis C umekumba watu milioni 12 wanaojidunga sindano za dawa za kulevya na kwamba homa hiyo ni chanzo cha vifo kuliko virusi vya Ukimwi duniani.