Wanandoa mkoani TABORA wametakiwa kuheshimu ndoa zao na kuepuka…

Wanandoa mkoani TABORA wametakiwa kuheshimu ndoa zao na kuepuka migogoro kwa kufuata kanuni na taratibu za sheria za dini.
Wakizungumza na CG FM,baadhi ya viongozi wa dini,Mchungaji EMMANUEL CHEREHANI wa kanisa la Moravian IPULI pamoja na mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu TANZANIA-BAKWATA,Shekhe RAJABU RASHIDI wamesema migogoro iliyopo katika ndoa inatokana na kukosa hofu ya Mungu.

Kwa upande wake Nabii wa kanisa la BETHEL,Nabii JACKSON MASATO amesema ndoa ni agano kutoka kwa Mungu na kwamba wanandoa wanatakiwa kuwa kupatana,kuaminiana na kujishusha.