Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Wataalamu wa silaha za sumu hawajapewa kibali kuingia Douma

  • April 17, 2018

Mwanadiplomasia wa Uingereza amesema Urusi na Syria wamewazuwiya wachunguzi wa shirika la kudhibiti silaha za sumu OCPW kuingia mjini Douma kuchunguza madai ya shambulizi la silaha za kemikali mjini humo.

Niederlande OPCW-Sondersitzung zu mutmaßlichem Giftgaseinsatz in Duma (Getty Images/AFP/K. van Weel)

Kulingana na balozi wa Uingereza nchini Uholanzi Peter Wilson, mkuu wa shirika la OCPW Ahmet Uzumcu, ameuambia mkutano wa hadhara kwamba wachunguzi wake wameshindWa kupata nafasi au ruhusa ya kuingia mjini Douma.

Wilson amesema Serikali ya Syria pamoja na Urusi wamewanyima nafasi wachunguzi hao kuingia mjini humo kwa sababu za kiusalama, amesema mpaka sasa bado hawajaweza kuhakikishiwa usalama wao na haijawa wazi ni lini hasaa hilo litakapofanyika.

Kundi hilo lilitarajiwa kuanza kazi hapo jana baada ya kuwasili mjini Damascus siku ya Jumamosi. Lakini badala yake walikutana na maafisa katika hoteli moja mjini humo na hakukuwepo na chombo chochote cha habari kilichokubaliwa kufuatilia mkutano huo. Hata hivyo Urusi na Syria wamekanusha madai ya kuwazuwiya wachunguzi hao kuingia mjini douma.

Aidha wataalamu wanadai kemikali ya Chlorine pamoja na Sarin zilitumika katika shambulizi hilo la douma mnamo Aprili 7 na kusababisha mauaji ya watu 40.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya watoa wito wa suluhu la kisiasa Syria

Huku hayo yakiarifiwa Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya wamesema wanaunga mkono juhudi zote zinazoweza kuizuwiya Syria kutumia silaha za sumu na kutoa wito wa kupatikana suluhu la kisiasa kwa mgogoro wa Syria uliyodumu miaka 7 sasa. Mwaziri hao 28 wamekosoa shambulizi la kijeshi linalioungwa mkono na Urusi kwamba serikali ya Syria inapigana dhidi ya waasi na kuitisha usitishwaji wa mapigano haraka ili kutoa nafasi ya upatikanaji wa misaada ya kiutu.

Luxemburg EU-Außenministertreffen (Getty Images/AFP/E. Dunand)

Katika taarifa ya pamoja baada ya mazungumzo mjini Luxembourg mawaziri hao wa Umoja wa Ulaya wamemlaumu rais Bashar al Assad kwa shambulizi la mjini Douma na kuunga mkono mashambulizi yaliyofanywa siku ya Jumamosi na Marekani Ufaransa na Uingereza siku ya Jumamosi linasemekana kuharibu hifadhi ya kemikali za sumu nchini Syria.

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema Umoja wa Ulaya umeungana katika wakati muhimu wa kutaka kulinda na kuondoa kabisa matumizi ya sialaha za kemikali.  Naye Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema shambulizi la majibu kutoka nchi za Magharibi lililofanyika siku ya jumamosi lilihitajika lakini wanachama wengine wa Umoja huo wamekuwa makini  kuzungumzia hilo ili kuepusha mgogoro uliyopo kupanuka zaidi.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

TABORA: Wananchi walalamikia zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa.
Wanariadha wengine watano wa Afrika wametoweka Gold Coast

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise