
Wazazi husababisha watoto kutosoma vizuri na usumbufu kwa walimu…
Wazazi wanaochelewa kuwapeleka watoto wao shule zinapofunguliwa wanasababisha wanafunzi kutosoma vizuri darasani na kuleta usumbufu kwa walimu.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ISIKE katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA,PAUL SONGORO amesema mahudhurio ya wanafunzi siku ya kwanza siyo ya kuridhisha kutokana na wazazi kuwasafirisha watoto wao kwenda mbali wakati wa likizo.
Kwa upande wake,Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo ya msingi,MARIAM JONATHAN amesema licha ya mahudhurio siku ya kwanza kuwa ya wastani lakini walimu wameanza rasmi kufundisha.
Hata hivyo wamewapongeza wazazi wa wanafunzi waliohudhuria masomo kwa sababu wamejitahidi kuwanunulia sare za shule,madaftari na viatu na kuwataka wazazi wengine waige mfano huo.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba waliokuwepo shuleni siku ya kwanza baada ya shule kufunguliwa TAUSI MUSA na ANANIA PIUS wamesema wamejiandaa vyema kukabiliana na mitihani iliyoko mbele yao.
Uongozi wa shule ya msingi ISIKE unatarajia kuitisha kikao cha wazazi baadaye wiki hii ili kuweka mipango madhubuti ya wanafunzi kupata chakula shuleni hatua ambayo itaongeza uelewa kwao na kupunguza utoro.