Wazazi na walezi mkoani TABORA wameaswa kufuatilia mienendo ya…

Wazazi na walezi mkoani TABORA wameaswa kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kufahamu kama wanapotoka nyumbani wanakwenda shuleni na maendeleo yao kimasomo.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani kata ya GONGONI,KESSY ABDULRAHMAN katika mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya ALI HASSAN MWINYI.
Amesema suala la wazazi na walezi kuzingatia mienendo ya wanafunzi wao ni muhimu ili kuondoa utoro wa kudumu.
Diwani KESSY amewaomba wazazi kushirikiana na walimu ili kupata taarifa ya mtoto pindi awapo shuleni huku akiwaasa wanafunzi wa kidato kwanza mpaka cha tatu kuwa na nidham darasani pamoja na kuzingatia masomo.