Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Wazazi wa Warmbier waeleza mateso yaliomkabili Korea kaskazini.

  • September 27, 2017

Wazazi wa Otto Warmbier wameelezea hali ya kutisha iliomkabili mtoto wao alipowasili nyumbani kutoka Korea kaskazini.

Fred na Cindy Warmbier wameliambia shirika la habari la Fox and Friends kuwa Watu wa Korea kaskazini ni “magaidi waliomtesa mtawalia” mtoto wao.

Mwanafunzi huyo wa Marekani alifungwa Pyongyang mnamo 2016 kwa kuiba kibandiko cha hoteli.

Aliachiwa kwa misingi ya matibabu mnamo Juni mwaka huu lakini aliwasili nyumbani akiwa mahututi na alifariki siku chache baadaye.

Korea kaskazini imekana daima kumtesa Warmbier. Inasema aliugua bakteria ya neva mwilini lakini madakatari wa Marekani hawakugundua bakteria yoyote.

‘Hii haikuwa ajali‘

Katika mahojiano yao ya kwanza tangu kufa kwake, wameliambia shirika la habari la Fox news kwamba “wanahisi umewadia muda kusema ukweli kuhusu hali iliyomkabili Otto”.

Madakatari Marekani walisema alikuwa katika hali ambayo mwili wake ulikuwa hauitikii, lakini familia ya Warmbiers wanasema kuita hali hii coma “sio haki”.

Bi Warmbier anasema walipomuona mtoto wao alikuwa “anazunguka na kufafatika kwa nguvu akitoa sauti isiyo ya binaadamu”.

Kichwa chake kilikuwa kimenyolewa, alikuwa kipofu na kiziwi, mikono na miguu yake ilijipinda na alikuwana alama kubwa ya jeraha mguuni mwake, alisema. “Ilikuwa ni kama mtu ameyavunja na kuyapanga upya meno yake ya chini”.

“Otto aliteswa mtawalia na kwa kusudi na Kim na utawala wake. Hii haikuwa ajali,” amesema bwana Warmbier.

Ameeleza kuwa mwanawe altengwa na familia yake, nchi yake, na dunia nzima nzima na kwamba serikali haikuwapa taarifa zozote kuhusu kifo chake.

Familia hiyo ilikataa afanyiwe upasuaji kubaini chanzo cha kifo kwasbabau wanasema walidhani kwamba ameteseka vya kutosha na “singeruhusu aondoke mbele ya macho yangu,” aliongeza

Ametoa wito kwa watu wasiende Korea kaskazini ,akieleza ni kuchezea propaganda za Pyongayang. Raia wa Marekani wamepigwa marufuku sasa kusafiri kwenda Korea kaskazini.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Serena Williams ajuta mtandaoni juu ya mwanaye wa kwanza.
Wananchi wa mkoa wa TABORA wametakiwa kutunza mazingira na kutumia njia mbadala za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Guardiola alinichukulia kama adui na…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise