
Waziri Aiagiza kamati ya ulinzi kufanya uchunguzi wa kuchomwa…
Agizo kwa kamati ya ulinzi na usalama wilayani NGORONGORO kuchuguza chanzo cha mgogoro wa kuchomwa moto kanisa. Naibu waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi WILLIAM OLE NASHA ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya NGOROGORO mkoani ARUSHA kuchunguza chanzo cha mgogoro ulisababisha kuchomwa moto kwa kanisa na kuvunjwa kwa ofisi ya kijiji cha KISANGIRO wilayani humo.
Amesema hayo wakati akikagua madhara aliyosababishwa na tukio hilo ambapo amewataka wananchi walioathirika kuwa wavumilivu wakati kamati inachunguza chanzo cha mgogoro huo.
INSERT……………. WILLIUM OLENASHA………….10”
Kwa upande wa viongozi wa kabila ambalo linaabudu kijadi wamesema wameathirika kwa kuchomwa eneo lao la kuabudia.
INSERT……………………. VIONGOZI KIMILA …………………10”
Naye mkuu wa wilaya ya NGORONGORO, RASHID TAKA amewaomba wananchi kurejea katika makazi yao waliyoyakimbia wakati wa tukio hilo ili kuendelea na shughuli zao za uzalishaji.