Zaidi ya shilingi Bilioni 23 na Milioni 200 zimetumika…

Zaidi ya shilingi Bilioni 23 na Milioni 200 zimetumika kunusuru kaya maskini na miradi mbalimbali ya maendeleo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini- TASAF)
Mratibu wa TASAF mkoa wa TABORA,NGOKO BHUKA katika taarifa yake kwa viongozi wa TASAF makao makuu amesema fedha hizo zimetumika kuanzia mwaka 2015 hadi Agosti mwaka huu.
Amesema wilaya ya UYUI ndiyo imenufaika zaidi kwa kupata zaidi ya shilingi milioni 562.
Naye Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wilaya ya UYUI,Daktari SHIJA MAIGE amesema kuwa fedha zote zilizotolewa na TASAF zilifika kwa walengwa kwa muda muafaka na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya hiyo huku akiomba walionufaika na mpango wa TASAF kutoondolewa kwenye mpango baada ya kuondokana na umaskini.
Akitoa maelekezo juu ya fedha hizo kuendelea kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa, mtaalam wa mafunzo na ushirikishwaji kutoka TASAF Makao Makuu,MECRY MANDAWA amesema TASAF ina lenga kuinua kaya maskini na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Naye Afisa Uwasilishaji Fedha,KWEJI KASULENDE amesema TASAF inakusudia kuinua zaidi vikundi vya wajasiriamali pamoja na vikoba ili kkufikia malengo yaliyokusudiwa.
Viongozi wa TASAF Makao Makuu wako katika ziara ya siku tatu mkoani TABORA kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini.