Klabu ya soka ya RHINO RANGERS ya mkoani TABORA…

Klabu ya soka ya RHINO RANGERS ya mkoani TABORA inashuka dimbani kesho kucheza na TRANSIT ya SHINYANGA katika mwendelezo wa ligi daraja la kwanza TANZANIA.
RHINO wanaingia katika mchezo wa kesho wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya ALLIANCE ya MWANZA ambapo walipoteza bao moja kwa bila huku TRANSIT wenyewe walipata alama moja baadq ya kutoka sare na JKT OLJORO ya mkoani ARUSHA.
Mchezo huo utaanza saa kumi na nusu jioni katika uwanja wa mwinyi na utatangazwa moja kwa moja na kituo hiki.