
TABORA: TAKUKURU yawaonya wanaotishia usalama wa wanawaripoti wala rushwa.
Mwandishi: Hamad Rashid.
Wananchi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwatishia maisha wanaowaripoti wameonywa kuwa watachukuliwa hatua za kisheria watakapobainika. Onyo hilo limetolewa na Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini-TAKUKURU wilayani UYUI,ROBERT KAHIMBA wakati akizungumza na wananchi wa kata ya GOWEKO katika mkutano wa hadhara.
Ameongeza kuwa sheria inabainisha kuwa endapo mhusika atafanya hivyo atatozwa faini na kifungo.
Alikuwa akijibu swali la mwananch wa GOWEKO,SELEMANI MUSA aliyehoji kinga ya mtoa taarifa za vitendo vya rushwa atakapojulikana kwa mtoaji au mpokea rushwa.
Naye Afisa wa TAKUKURU,JUMA SWALEHE kutoka Makao Makuu ya TAKUKURU amesema ni jukumu la kila mwananchi kutoa taarifa za wanaojihusisha na vitendo vya rushwa katika jamii bila woga wowote.