
TABORA: MILAMBO FC na JKT MSANGE Uso kwa Uso…
Timu za MILAMBO FC na JKT MSANGE zote za TABORA zitakuwa katika wakati mgumu keshokutwa wakati zitakapokutana katika mchezo wa mwisho wa Ligi Daraja la Pili TANZANIA BARA.
Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa ALI HASSAN MWINYI na utakuwa ni wa mwisho huku JKT MSANGE ikiwa na alama 11 wakati MILAMBO ina alama kumi na zote zina nafasi ya kupanda ligi daraja la kwanza.
MILAMBO au JKT MSANGE mojawapo ikishinda mchezo huo itapaswa kuomba klabu ya MASHUJAA ya KIGOMA ipoteze mchezo wake dhidi ya AREA C ya DODOMA watakapokutana.
AREA C ina alama 15,MASHUJAA alama 12,JKT MSANGE alama 11 na MILAMBO alama 10.
Baada ya kuitoa klabu ya MAJIMAJI RANGERS ya LINDI katika mashindano ya Kombe la Shirikisho,klabu ya MTIBWA SUGAR ya MOROGORO itasafiri kuelekea Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi zake tatu za Ligi Kuu ya VODACOM TANZANIA BARA.
Msemaji wa kikosi cha MTIBWA,TOBIAS KIFARU amesema baada ya kumaliza mechi hizo watarejea mjini MOROGORO.
MTIBWA SUGAR inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu kwa alama zao 26