
7 wauawa katika mapambano na Polisi Ethiopia
Watu saba wamekufa huko Ethiopia kaskazini baada ya vikosi vya usalama kufyatua risasi kwenye mkusanyiko wa watu waliohudhuria tamasha la kidini siku ya jumamosi.
Vifo hivyo katika mji wa Waldiya vimesababisha maandamano ya siku mbili yaliyosababisha uharibu wa nyumba, magari na barabara kufungwa .
Mashuhuda wanasema shida ilianza siku ya jumamosi pale waumini hao walipoanza kuimba nyimbo za kuipinga serikali na ndipo vikosi vya serikali vilianza kuwafyatulia risasi na kusababisha majeraha na vifo.
Waandamanaji wenye hasira walianza kuchoma magari,nyumba na biashara za wale wanaodhaniwa kuunga mkono serikali.Waandamanaji kadhaa wanashikiliwa na Polisi.