
Serikali imewataka vijana nchini kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo ajira…
Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira,ANTHONY MAVUNDE amewataka vijana nchini kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo ajira kwa kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri ili kupunguza tatizo hilo nchini.
Akizungumza mkoani ARUSHA katika mkutano mkuu wa vijana kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki ambao umekutanisha mamia ya vijana, MAVUNDE amesema serikali imeweka mipango mizuri ya kusaidia vijana.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa GEITA,UPENDO PENDEZA amesema huu ni wakati ambao vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya jamii.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais- TAMISEMI,JOSEPH KAKUNDA amewaagiza maafisa afya wa ngazi zote katika halmashauri,hospitalini,kata na vijiji kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kuwa na vyoo bora kwenye kaya zao pamoja na kuvitumia ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza miongoni mwa jamii.
Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano wa siku tano wa Chama cha Afya ya Jamii TANZANIA unaofanyika katika Hoteli ya KATALA BEACH mjini SINGIDA.
Akizungumzia shule za msingi na sekondari,Naibu Waziri KAKUNDA amebainisha kuwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa,kila wanafunzi 20 wa kike hutumia tundu moja la choo na wanafunzi 25 wa kiume wanatumia pia tundu moja,kiwango ambacho hakitoshelezi mahitaji kutokana na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule hizo.
Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa mkoa wa SINGIDA,Daktari SELEMANI MANYATA amesema kuwa karibu asilimia nne ya wananchi wa mkoa wa SINGIDA ambao ni sawa na watu 11,000 hawana kabisa vyoo bora na asilimia 48 ya wananchi wana vyoo vya muda hali ambayo inachangia uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji yanayoleta magonjwa ambayo matibabu yake ni gharama kubwa.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Afya ya Jamii TANZANIA,Daktai MASHOMBO MKAMBA amesema baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na watu kuelewa na kuwa tayari kupima afya zao kwa sababu mpaka sasa bado watu ni wagumu kupima afya zao.