Anthony Joshua kuvaana na Carlos Takam Oktoba 28

Bondia Anthony Joshua anatarajiwa kutetea mataji yake ya IBF na WBA atakapovaana na Carlos Takam baada ya Kubrat Pulev kujitoa kufuatia majeraha.
Pambano hilo linalotarajiwa kuwa kali na la kuvutia litapigwa Oktoba 28 katika dimba la Cardiff ambapo mpaka sasa tiyari tiketi 70,000 zimeshauzwa.
Litakuwa pambano la kwanza la Joshua tokea alipomtwanga Wladimir Klitschko katika dimba la Wembley April.

Pulev alipata majereha ya bega wakati akijiandaa na mchezo huo.
Takam mzaliwa wa Cameroon na anayeishi nchini Ufaransa ana miaka 36 na anatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Joshua.