ANTONIO GUTERRES amesema lengo la dunia isiyo na silaha…

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bwana ANTONIO GUTERRES amesema lengo la dunia isiyo na silaha za nyuklia linahitaji juhudi za kimataifa
Katibu Mkuu GUTERRES amesema hayo katika mkutano wa ngazi ya juu wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza silaha za nyuklia mjini NEW YORK akisisitiza kuwa dunia yenye usalama ni dunia isiyo na silaha yoyote ya nyuklia.
Amesema ingawa hivi karibuni lengo hilo limekumbwa na changamoto kadhaa, yakiwemo majaribio ya nyuklia na makombora yaliyorushwa na KOREA KASKAZINI.
Bwana GUTERRES amesema nchi zenye silaha za nyuklia zinabeba jukumu maalumu la kuongoza kwa kuchukua hatua imara,ikiwemo kutekeleza mikataba mbalimbali ya kutoeneza silaha za nyuklia.