
Bilioni 622 na Milioni 733 zatumika kunusuru kaya maskini
Zaidi ya shilingi Bilioni 622 na Milioni 733 zimetumika kunusuru zaidi ya kaya maskini milioni moja hapa nchini kati ya mwaka 2013 na Februari mwaka huu.
Meneja wa Mpango wa Kuweka Akiba na Kukuza Uchumi wa Kaya Maskini kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini –TASAF-,TATU MWARUKA amesema miongoni mwa fedha hizo zimetumika kwa ajili ya usimamizi katika ngazi mbalimbali za halmashauri na mkoa.
Mpango wa TASAF wa kunusuru kaya maskini unahakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanakwenda sambamba na watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanapelekwa kliniki.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini- TASAF inatekeleza sehemu ya nne ya mpango wa kunusuru kaya maskini katika wilaya ya UYUI lengo likiwa ni kuwawezesha walengwa kujua taratibu za kujiwekea akiba kimaendeleo.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa TASAF wilaya ya UYUI,BAINAS KAMBIMBAYA amesema kazi iliyopo kwa sasa ni kuendelea kuhamasisha walengwa ili kuunda vikundi na kuimarisha uchumi wa kaya zao.
Walengwa wa mpango wa TASAF wa kunusuru kaya maskini wanesisitizwa kuzitumia kwa usahihi fedha wanazopata ili kuondokana na umaskini.