
CARITAS Lakabidhi gati la maji Ndevelwa.
Zahanati ya kijiji cha NDEVELWA katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA kukabidhiwa gati la maji ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji.
Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Kanisa Katoliki –CARITAS –Jimbo Kuu la TABORA, limekabidhi gati la maji lenye thamani ya shilingi milioni 13 katika zahanati ya NDEVELWA,Manispaa ya TABORA ili kumaliza tatizo la ukosefu wa maji katika zahanati hiyo.
Akikabidhi gati hilo kwa serikali ya kijiji cha NDEVELWA,Mkurugenzi wa CARITAS TABORA, Padri ALEX NDUWAYO amesema baada ya kugundua kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa maji katika zahanati hiyo waliamua kutoa msaada wa kujenga gati hilo.
Kwa upande wake,Diwani wa kata ya NDEVELWA,SELEMAN MAGANGA ameishukuru CARITAS na kwamba sasa tatizo la ukosefu wa maji limemalizika kwa sababu gati hilo lina uwezo wa kuhifadhi lita elfu 55 za maji.
Naye Mganga Mfawidhi wa zahanati ya NDEVELWA,JAPHET HOSA amesema kipindi cha nyuma wagonjwa walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa CARITAS,Idara hiyo ya maendeleo ya jamii ya Kanisa Katoliki inaendelea kushirikiana na serikali katika miradi mbalimbali ya imaendeleo ili kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi wa TABORA.