CHAD yamkosoa Rais DONALD TRUMP wa Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya CHAD imewasilisha kwa balozi wa MAREKANI malalamiko na ukosoaji wake kuhusu amri dhidi ya uhamiaji iliyotolewa hivi karibuni na Rais DONALD TRUMP wa nchi hiyo
Mbali na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya CHAD kulalamikia hatua hiyo imemwita Balozi wa MAREKANI nchini humo,Bwana GEETA PASI na kuonyesha masikitiko yake kuhusiana na hatua ya Rais TRUMP ya kuijumuisha CHAD kupitia amri dhidi ya uhamiaji.
Kufuatia hatua hiyo serikali ya CHAD imeitaja hatua hiyo kuwa isiyo ya uadilifu na ya kushangaza.
Wizara hiyo imewahutubu viongozi wa MAREKANI ikisema uamuzi huo wa MAREKANI hauwezi kutetewa.
Awali Bwana GEETA PASI,Balozi wa MAREKANI nchini CHAD alikuwa amedai kuwa hatua hiyo ya kuijumuisha nchi hiyo ya Afrika katika amri hiyo,haitakuwa na athari yoyote mbaya katika uhusiano wa CHAD na MAREKANI.