Chemchem, TABORA: Dimbwi la maji barabarani lahatarisha maisha ya…

Wakazi wa mtaa wa KALAMATA katika kata ya CHEMCHEM,halmashauri ya Manispaa ya TABORA wamelalamikia kuwepo kwa dimbwi lililojaa maji katika barabara ya SABASABA inayokarabatiwa katika mtaa huo hali inayohatarisha usalama wa wakazi hao hasa watoto.
Baadhi ya wakazi hao BERNAD ALBANO na JUSTINE JULIUS wamesema dimbwi hilo limekuwa kero kwao na mpaka sasa watu watano wametumbukia katika dimbwi hilo.
CG FM imemtafuta mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa KALAMATA,Mufti HAMIDU RASHID ambaye amekiri dimbwi hilo kuwa ni kero kwa wakazi hao.