Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Chuo Kikuu cha Nairobi chafungwa kwa sababu za kiusalama.

  • October 3, 2017
Bango la UoN.

Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya kile ambacho viongozi wa chuo hicho wamesema ni haja “kudorora kwa hali ya kiusalama” chuoni humo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya siku kadha za wasiwasi uliotokana na makabiliano kati ya wanafunzi na polisi wa kukabiliana na fujo ndani ya chuo hicho.

“Wanafunzi wote wametakiwa kuondoka vyumba vyao vya malazi mara moja kabla ya saa tatu asubuhi,” taarifa ya seneti ya chuo hicho imesema.

Polisi wakiwa mkabala na wanafunzi waliokuwa wakiandamana chuoni hapo.

Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino.

Polisi wakikabiliana na mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakiandamana.

Bw Owino, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.

Baadaye alikamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mengine ya kumshambulia mpiga kura wakati wa uchaguzi mwezi Agosti.

Aliachiliwa kwa dhamana.

Wanafunzi takriban 26 walijeruhiwa. Video ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni zimeonyesha maafisa wa polisi wakiwafurusha wanafunzi kutoka kwa vyumba vya malazi na hata kwenye madarasa.

Wanafunzi wa UoN wakiwa wanatoka chuoni baada ya kufungwa kwa chuo chao.

Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema kufikia sasa ni vigumu kubaini iwapo video hizo ni za kweli na iwapo wanaoonekana wakipigwa na maafisa wa polisi ni wanafunzi.

Mamlaka inayosimamia utendakazi wa polisi na kutetea haki za raia (IPOA) imetoa wito kwa wanafunzi 26 ambao walijeruhiwa kuandikisha taarifa.

“Kuandikishwa kwa taarifa hizi kutatusaidia kuharakisha uchunguzi,” taarifa ya IPOA iliyotiwa saini na afisa mkuu mtendaji Dkt Joel Mabonga imesema.

Awali, taarifa ya mwenyekiti wa IPOA Macharia Njeru ilikuwa imesema: „Ni kweli wapo wanafunzi ambao walijeruhiwa na baadhi ya maafisa wa polisi walipokuwa wanakabiliana na waandamanaji. Kufikia sasa, hatujapokea ushahidi wowote wa kuonesha kunaye aliyefariki.”

Bw Njeru alisema baada ya uchunguzi, wamebaini nyingi za video na picha ambazo zinaenezwa mtandaoni zikidaiwa kuwaonesha polisi wakiwashambulia wanafunzi ni za uzushi.

 

 

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Watu wengi wapigwa risasi mjini Las Vegas
Mkuu wa Mkoa wa Tabora aagiza makampuni ya uzalishaji,usambazaji na ununuzi wa pamba mkoani TABORA kuhakikisha yanatoa mbegu na dawa bora.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Guardiola alinichukulia kama adui na…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise