FIFA HAIMTAMBUI LUKAKU KUWA MFUNGAJI WA MUDA WOTE UBELGIJI.
Baada ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA kufuta matokeo ya Mchezo wa kirafiki kati ya Ubelgiji dhidi ya Luxembourg hali hiyo imebadili rekodi ya Romelu Lukaku kuwa Mfungaji wa muda wa Timu hiyo.
FIFA imefuta matokeo ya mchezo huo baada ya kocha wa Ubelgiji kufanya mabadiliko ya wachezaji saba badala ya Sita ambayo ni kinyume na sheria za FIFA hivyo matokeo wala Magoli ya Mchezo huo hayatahesabika.
Mchezo huo ambao Lukaku alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 5-3 na kumfanya nyota huyo kuwa na magoli 30 kabla ya kufunga goli dhidi ya Japan na kumfanya Mfungaji wa muda wote ndani ya Ubelgiji akifikisha magoli 31 lakini kwa sasa anatambulika kuwa na Magoli 28.
Mpaka sasa rekodi ya Mfungaji bora wa muda wote katika Timu ya Taifa ya Ubelgiji kwa mujibu wa FIFA inashikiliwa na Bernard Voorhoof pamoja na Paul van Himst wenye magoli 30 kila mmoja.
Lukaku atalazimika kusubiri mpaka mwezi Machi Mwakani 2018 wakati wa mechi za Mwisho kabla ya Kombe la Dunia kuanza.