Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia

  • December 29, 2017December 29, 2017

George Weah Leo atatangazwa kuwa Rais wa Liberia na tume ya uchaguzi nchini humo baada ya kuongoza kwa asilimia 61.5 kati ya kura asilimia 98.1 zilizohesabiwa.

Bwana Weah amemtangulia mpinzani wake Joseph Boakai kwa kura asilimia 60.

Anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kupata kiongozi kwa njia ya kidemokrasia baada ya matokeo kutangazwa.

“Ninaelewa umuhimu na majukumu ya kazi kubwa niliyokabidhiwa leo. Mabadiliko yanakuja.”

Bi Johnson Sirleaf alimshinda George Weah, katika uchaguzi wa mwaka 2005, na kuchukua madaraka mwaka uliyofuata baada ya kuisha kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyopelekea Rais Charles Taylor kutolewa madarkani na waasi.

Taylor sasa amefungwa kwa miaka 50 nchini Uingereza baada ya kuhukumiwa kwa vitendo vya uhalifu nchini Sierra Leone.

Kampeni ya Bw Weah, chini ya muungano wa mabadiliko ya demokrasia, uliolenga kura ya vijana wakati mpinzani wake makamu wa rais Boakai alionekana kupitwa na wakati na kutokuwa na mashiko.

Lakini uchaguzi wa Weah haukwenda bila mvutano, kwa kuwa mgombea mwenza alikuwa Jewel Taylor mke wa zamani rais aliyefungwa Charles Taylor.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Tume ya UKIMWI ZANZIBAR inakusudia kuongeza elimu kwa makundi hatarishi na vijana ili kuhakikisha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI yanapungua
Rais Trump aishutumu China kwa kukiuka vikwazo vya UN dhidi ya Korea Kaskazini

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise