
GUARDIOLA awataka wachezaji wa timu hiyo kujifunza kwa Liverpool
Kocha Mkuu wa klabu ya soka ya MANCHESTER CITY,PEP GUARDIOLA amewataka wachezaji wa timu hiyo kujifunza katika kichapo cha mabao manne kwa matatu waliyofungwa jana usiku na timu ya soka LIVERPOOL katika ligi kuu soka nchini UINGEREZA.
GUARDIOLA amesema kichapo cha jana kinafaa kuwa fundisho kwa wachezaji hao ili kujiimarisha zaidi kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa UINGEREZA.
MAN CITY ilikuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote katika ligi kuu soka nchini UINGEREZA lakini jana wameonja joto la jiwe kwa mara ya kwanza kwa kipigo cha mabao manne kwa matatu.