Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoani TABORA imempongeza…

Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoani TABORA imempongeza Rais JOHN POMBE MAGUFULI kwa kazi nzuri ya kusimamia raslimali za nchi yetu na kuhakikisha zinatumika vizuri kwa manufa ya watanzania na vizazi vijavyo.
Taarifa iliyotolewa mwishoni mwa kikao chake maalum,halmashauri kuu hiyo imesema CCM mkoa wa TABORA inaunga mkono jitihada zote za serikali ya Awamu ya Tano katika kuimarisha uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya Watanzania.
Halmashauri Kuu ya CCM hali kadhalika imempongeza Rais kwa uteuzi wa mawaziri wanaotoka mkoa huu ambao ni Dakari HAMISI KIGWANGALA- Mbunge wa NZEGA vijijini kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na JOSEPH KAKUNDA -Mbunge wa SIKONGE kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI.
Kikao hicho licha ya kuwapongeza wabunge wote wa mkoa wa TABORA kwa jinsi wanavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM pia kimewataka kuhakikisha wanatimiza ahadi zote walizoahidi wananchi wa majaimbo yao ili iwe rahisi kwa ushindi wa CCM mwaka 2019 wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu.
Chama cha Mapinduzi mkoa wa TABORA kimeipongeza serikali kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kusimamia vyama vya msingi vya tumbaku na kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Pia kimeitaka serikali kuharakisha mpango wa ununzi wa tumbaku ambayo bado ipo mikononi mwa wakulima ili kuwainua kiuchumi na kuwawezesha kujiandaa vizuri na msimu unaoanza wa kilimo.