
Halmashauri ya manispaa ya TABORA imeshindwa kukusanya asilimia 50…
Halmashauri ya manispaa ya TABORA imeshindwa kukusanya asilimia 50 ya mapato ya ndani katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2017-2018 na badala yake imekusanya asilimia 38 peke yake.
Akizungumza katika kikao cha mapendekezo ya rasimu ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2018-2019 ya shilingi Bilioni 61.4,Mchumi wa Manispaa ya TABORA, JOHANNES KILONZO amesema wameshindwa kufikia lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake,Meya wa Manispaa ya TABORA,LEOPARD ULAYA amesema kikao cha kujadili mapendekezo ya bajeti kipo kwa mujibu wa sheria.
Naye Mkuu wa wilaya ya TABORA,Mwalimu QUEEN MLOZI amesema katika mwaka wa fedha 2016-2017 halmashauri hiyo ilikuwa na hoja ya kujibu na kuwataka mwaka kuhakikisha katika mwaka huu wa fedha wasije na majibu yale yale.
Amesema wanashikamana katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia asilimia 80 na hivyo kusaidia kuleta maendeleo katika wilaya ya TABORA
Akizungumza katika kikao hicho,Diwani wa kata ya NG’AMBO,GEORGE MPEPO ameunga mkono kauli ya mkuu wa wilaya ya TABORA ya kuhakikisha wanaongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya TABORA limepitisha kwa kauli moja mapendekezo ya bajeti ya shilingi Bilioni 61 na milioni 400 kwa ajili ya mwaka wa fedha 2018-2019.