Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Halmashauri zote za wilaya mkoani TABORA zimeagizwa kutumia wanachuo…

  • October 12, 2017
Chuo Cha ardhi kinavyoonekana kwa nje.

Halmashauri zote za wilaya mkoani TABORA zimeagizwa kutumia wanachuo wa chuo cha Ardhi katika kupima viwanja kutokana na kuwepo na upungufu wa watumishi wa idara ya Ardhi katika halmashauri hizo.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Daktari ANGELINA MABULA wakati akizungumza na watumishi wa chuo cha Ardhi na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA.

Amesema kuna tatizo la watumishi katika sekta ya ardhi lakini halmashauri zimekuwa zikishindwa kuw tumia wataalamu wa chuo cha Ardhi TABORA jambo ambalo lingepunguza tatizo lililopo la upimaji ardhi.

Kwa upande wake,Mkuu wa chuo cha Ardhi TABORA,BISEKO MUSIBA amesema wanachuo wengi wamekuwa wakishindwa kufanya kazi zao kwa ufanisI wanapokwenda kwenye mazoezi kutokana na vifaa kuwa na bei kubwa na kusababisha wshindwe kumudu gharama hizo.

Naye mkuu wa wilaya ya TABORA,Mwalimu QEEN MLOZI amesema maagizo ya Naibu Waziri huyo wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi atayafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuelekeza idara ya ardhi kuwatumia wanachuo hao wenye utaalam katika sekta ya upimaji viwanja.

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maelendeleo ya Makazi amesema wizara itakapotangaza nafas za kazi wanachuo wataajiriwa kutokana na uzoefu walionao katika sekta hiyo.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Jeshi la polisi mkoani TABORA limesema matukio ya mauaji yamepungua kwa asilimia 37.
Watu WATANO wamekufa kutokana na mvua zilizonyesha katika kata ya NANGA wilayani IGUNGA

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise