Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Hospitali ya Misheni Rulenge yaomba msaada kuokoa maisha ya…

  • November 9, 2017

Ngara. Majeruhi 43 wa bomu lililolipuka katika Shule ya Msingi Kihinga wilayani Ngara mkoani Kagera, ambao wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Rulenge baadhi wanahitaji kuongezewa damu ili kuokoa maisha yao. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Dk Revocatus Ndyekobora amesema kati ya majeruhi hao, wanafunzi ni 42 na mwalimu wao wa darasa wanahitaji uniti 50 za damu. “Tayari wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Alfred Rulenge inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge wamechangia uniti 46 za damu kusaidia wenzao,” amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo leo Alhamisi Novemba 9,2017 asubuhi, Dk Ndyekobora amesema timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera imewasili Ngara kusaidiana na wenzao kuwafanyia uchunguzi na kuwatibu majeruhi hao. “Watakaobainika kuhitaji huduma maalumu watahamishiwa hospitali zingine kulingana na taarifa ya madaktari,” amesema Dk Ndyekobora.

Mbali ya damu, majeruhi pia wanahitaji mashuka na mablanketi zaidi ya 50 kutokana na yaliyopo kutotosheleza mahitaji. Amesema baadhi wamelazimika kulala sakafuni kutokana na vitanda kujaa. “Msaada wa chakula pia unahitajika kwa ajili ya majeruhi hawa ambao wametoka maeneo ya mbali kiasi cha kutowezesha wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kuwaletea chakula,” amesema Dk Ndyekobora.

Wanafunzi watano wafariki, 18 wajeruhiwa kwa mlipuko.Usafiri kwa ajili ya kuwahamishia hospitali zingine pia ni miongoni mwa mahitaji ya dharura yanayohitajika kuokoa maisha ya majeruhi hao. Amesema baadhi wamebainika kuwa na vipande vya vyuma vilivyotokana na mlipuko wa bomu uliotokea jana Jumatano Novemba 8,2017 wakati wanafunzi hao wa darasa la kwanza wakiingia darasani.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Aidan Bahama amepiga marufuku biashara ya vyuma chakavu katika maeneo ya shule akionya kuchukua hatua dhidi ya mwalimu mkuu na wakuu wa shule watakaobainika kuruhusu biashara hiyo. Amri ya Bahama imetokana na uchunguzi wa awali wa polisi kubaini mwanafunzi mmoja aliokota bomu na kulihifadhi kwenye begi lake kwa lengo la kuliuza kama chuma chakavu.

Wanafunzi waliopoteza maisha wafikia 6, majeruhi 42 Halmashauri kugharamia mazishi Bahama amesema halmashauri imechukua dhamana ya kugharimia majeneza na shughuli za mazishi ya watoto watano waliokufa katika tukio hilo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Nkilamachumu na mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ngara, George Lubagola wameiomba Serikali kuimarisha ulinzi na ukaguzi kwa watu wanaingia nchini kutoka Burundi ili kudhibiti uingiaji holela wa silaha na mabomu ya kutupa kwa mkono. Kijiji cha Kihinga ni miongoni mwa maeneo yanayopakana na nchi jirani za Burundi na Rwanda na kuna mwingiliano wa watu katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Mkurugenzi Halmashauri ya Tunduru ang’olewa.
Rais Magufuli avipa masharti Viwanda vya Sukari.

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise