Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Ivana Trump: Melania ajibizana na mke wa zamani wa…

  • October 10, 2017
Ivana Trump na Melania Trump.

Msemaji wa Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump ameeleza tamko la mke wa zamani wa Donald Trump Ivana kuwa “ya kujitafutia makuu na kelele za kutaka kujifurahisha”.

Ivana Trump alikuwa amesema kwenye kipindi cha Good Morning America cha runinga ya ABC kwamba yeye ni “kimsingi mke wa kwanza wa Trump, mimi ni mama wa taifa”.

Alisema huwa ana namba ya simu ya moja kwa moja White House lakini kwamba huwa hataki kupiga simu mara kwa mara huko kwa sababu hangependa kusababisha “wivu wa aina yoyote”.

Mke huyo wa kwanza wa Trump anavumisha kitabu chake kwa jina Raising Trump(Kumlea/Kumuinua Trump), ambacho kitaanza kuuzwa Jumanne.

Aliolewa na Donald Trump mwaka 1977 lakini walitalakiana miaka ya 1990 baada ya Trump kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye angekuwa mke wake wa pili, Marla Maples.

Ivana na Donald walijaliwa watoto watatu – Donald Jr, Ivanka na Eric Trump.

Ivana Trump aliambia GMA kwamba huwa anawasiliana na mume wake wa zamani angalau mara moja kila wiki mbili.

“Nina namba ya simu ya moja kwa moja White House, lakini huwa sitaki kumpigia (Trump) akiwa huko kwa sababu Melania yuko huko,2 amesema.

“Sitaku kusababisha aina yoyote ya wivu au jambo kama hilo kwa sababu kimsingi mimi ni mke wa kwanza wa Trump. Mimi ni mama wa taifa, Sawa?”

Melania Trump alijibu kwa ukali kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephanie Grisham.

“Bi Trump ameifanya ikulu ya White House kuwa nyumbani kwa [mwanawe wa kiume] Barron na Rais,” taarifa hio imesema.

“Hupenda sana kuishi Washington, DC na anachukulia kuwa heshima kubwa kwake kuwa Mama wa Taifa wa Marekani. Anapanga kutumia cheo na majukumu yake kuwasaidia watoto, na si kuuza vitabu.

“Ni wazi kwamba hakuna chochote cha maana kutoka kwa mke wake huyo wa zamani. Inasikitisha kwamba anajitafutia tu makuu na kutaka kelele za kutaka kujifurahisha kwa kelele zake mwenyewe.”

Majibizano hayo ni ya kwanza kutokea hadharani kati ya mke wa zamani wa rais na Mke wa Rais.

Kabla ya Trump, Ronald Reagan alikuwa rais pekee ambaye aliwahi kumpa talaka mke wake.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Jackie Chan athibitisha ujio wa filamu ya ‘Rush Hour 4’
Wanandoa mkoani TABORA wametakiwa kuheshimu ndoa zao na kuepuka migogoro kwa kufuata kanuni na taratibu za sheria za dini.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise