
Jamii mkoani TABORA imeshauriwa kukata kucha mara mbili kwa…
Jamii mkoani TABORA imeshauriwa kukata kucha mara mbili kwa wiki na kutozikata kwa kutumia mdomo kwa sababu kunasababisha hatari ya kuugua magonjwa ya kuhara.
Daktari wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa TABORA-KITETE kitengo cha afya ya uzazi na kizazi ,Daktari MNUBI BAGUMA amesema mtu akiwa na kucha ndefu hata kama atanawa maji mengi hataweza kumaliza bakteria waliopo ndani ya kucha zake.
Kwa upande wao,baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA BOSCO JOSEPH,SAID RAMADHAN na JOSEPH DEUS wameomba elimu zaidi iendelee kutolewa ili jamii ielewe madhara yatokanayo na kutonawa mikono kwa ufasaha.
Nao watoa huduma wa afya ngazi ya jamii MARY BALAZI na DAVID KANOLA wamesema wanahakikisha wananawa mikono kabla na baada ya kumhudumia mgonjwa ili kuua vijidudu na kuepusha kuhamisha wadudu kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mwingine.
Daktari BAGUMA ameitaka jamii kujiepusha na kula hovyo barabarani kwa sababu kufanya hivyo kunaongeza uwezekano mkubwa wa kula uchafu kwa sababu mtu hawezi kujui mazingira yalitumika kuandaa chakula au matunda hayo.