Jamii mkoani TABORA imetakiwa kujitoa kwa hali na mali…

Jamii mkoani TABORA imetakiwa kujitoa kwa hali na mali kushiriki katika kuboresha elimu na mkoa wa TABORA kwa jumla.
Wito huo umetolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa Mpango wa kuboresha elimu TANZANIA- EQUIP,MWANAIDI MSANGI akisema ushirikiano wa jamii katika elimu ni lazima uwe mkubwa ili kufikia malengo ya kuwa na maendeleo mazuri ya elimu.
Naye Afisa Elimu mkoa wa TABORA,SUZAN NYARUBAMBA amesema mpango wa kuboresha elimu TANZANIA- EQUIP umewapa nafasi walimu wa taaluma,walimu wakuu na walimu wakuu wasaidizi kusimamia kwa weledi maendeleo ya shule.