
Jeshi la polisi mkoani Tabora limewapongeza wananchi
Jeshi la polisi mkoani Tabora limewapongeza wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kukabiliana na uhalifu.
Akizungumza katika kongamano la ulinzi na usalama ukumbi wa ISIKE MWANAKIYUNGI mjini TABORA, kamanda wa polisi mkoa wa Tabora kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema wanapata ushirikiano kutoka kwa wananchi na kuongeza ufanisi katika jeshi hilo.
Kamanda MUTAFUNGWA Pia amesema wanaendelea kushirikiana na viongozi wa dini ili kuwashawishi wananchi kuachana na imani potofu za kishirikina.