
Jeshi la polisi mkoani TABORA limewataka madereva kufuata sheria
Jeshi la polisi mkoani TABORA limewataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamojana na kuepuka ulevi kwani ndiyo chanzo cha ajali.
Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema dereva anapotumia kilevi akiwa kazini anahatarisha maisha yake na abiria.
Pia Kamanda MUTAFUNGWA amewataka wamiliki wa vilabu vya pombe na Bar kuzingatia muda halali wa kufanya biashara zao kama leseni zao zinavyowaelekeza.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa MASEMPELE kata ya NG’AMBO mjini TABORA SHABAN KAOMBWE amesema kuwa kuna wauzaji wa pombe za kienyeji wasiotambulika na serikali nakuwataka wafuate sheria za biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda wa kufungua na kufunga.
Dereva wa bodaboda , PASCO JOHN amewasihi madereva wenzake wa vyombo vya usafiri kuwa makini na kazi zao kwa kuepuka ulevi kwani ni chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo yao.
Hata hivyo, jeshi la polisi nchini linahimiza kila abiria kuwa na mwamko wa kutoa taarifa pindi anapobaini dereva wa chombo husika cha usafiri ametumia kilevi au anaendesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali zinazoepukika.