
Jeshi la polisi mkoani TABORA linaendelea na uchunguzi wa…
Jeshi la polisi mkoani TABORA linaendelea na uchunguzi wa matukio mawili tofauti ya kujeruhi.
Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA,Kamishna Msaidizi Mwandamizi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la JOSEPH LUKASI,mkazi wa kitongoji cha UHEMELI,kata ya NDALA wilayani NZEGA amejeruhiwa vibaya katika sehemu zake za siri na kitu chenye ncha kali akiwa nyumbani kwake na mtu asiyejulikana.
Ameongeza kuwa katika tukio hilo watu kadha wamekamatwa na wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Katika tukio la pili,mtu mmoja KULWA JACKSON,mkazi wa kijiji cha IZIMBILI, kata ya UYUMBU wilayani URAMBO amejeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake baada ya kuvamiwa akiwa nyumbani kwake.
Kufuatia tukio hilo Kamanda MUTAFUNGWA amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo ni ugomvi wa urithi wa shamba.
Ameongeza kuwa uchunguzi wa jeshi la polisi unaonesha kuwa matukio ya kuheruhi yameanza kujitokeza katika mkoa wa TABORA.