
Jumapili hii ni NIGERIA vs MOROCCO katika michuano ya…
Timu ya Taifa ya NIGERIA itakutana na wenyeji MOROCCO katika fainali ya C kwa wachezaji wanaocheza katika bara la AFRIKA-CHAN itakayochezwa Jumapili wiki hii.
Hiyo ni baada ya timu zote kushinda mechi zao za Nusu Fainali jana, MOROCCO wakiwatoa jirani zao,LIBYA na NIGERIA wakiwatoa SUDAN ambapo NIGERIA ilipata ushindi wa bao moja kwa sifuri huku MOROCCO ikishinda mabao matatu kwa moja.
Mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu utachezwa keshokutwa kwa LIBYA na SUDAN kupambana kuanzia saa nne usiku huku pia mchezo wa fainali ukichezwa muda huo huo.