
Jumla ya watoto KUMI NA MMOJA wamezaliwa Siku ya…
Jumla ya watoto KUMI NA MMOJA wamezaliwa Siku ya Mwaka Mpya katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa TABORA- KITETE.
Muuguzi Kiongozi wa wodi ya Wazazi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa TABORA,ELIWAMPUKA MBWANA amesema kuwa watoto hao wamezaliwa kati ya mkeshawa Mwaka Mpya hadi Jumatatu usiku.
Bi ELIWAMPUKA amesema kati ya wanawake 11,SABA kati yao wamejifungua kawaida na WANNE wamejifungua kwa njia ya upasuaji na hakuna Mama wala mtoto aliyefariki dunia.