Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Juventus wachapwa baada ya kumpumzisha Gianluigi Buffon.

  • November 20, 2017
Gianluigi Buffon (kati) amecheza mechi 627 Serie A , 20 nyuma ya rekodi ya Paolo Maldini

Gianluigi Buffon aliachwa kwenye benchi Juventus walipokuwa wanacheza dhidi ya Sampdoria, hatua ambayo huenda iliwagharimu Jumapili.

Walipokezwa kichapo cha 3-2.

Buffon aliwekwa kwenye benchi pamoja na beki Andrea Barzagli, kwa sababu wanahitaji “muda kusahau” masaibu ya kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Massimiliano Allegri aliwapumzisha wawili hao, ambao tayari wamestaafu soka ya kimataifa, baada ya Italia kushindwa na Sweden mechi za muondoano wa kufuzu.

Sampdoria waliongoza kupitia bao la kichwa la Duvan Zapata, Lucas Torreira na Gianmarco Ferrari nao wakaongeza na kufanya mambo 3-0.

Gonzalo Higuain na nguvu mpya Paulo Dybala walikomboa mawili dakika za mwisho.

Juventus wamesalia alama nne nyuma ya viongozi wa ligi Napoli ambao bado hawajashindwa.

Inter Milan waliwapiku na kuingia nafasi ya pili baada ya kuwashinda Atalanta 2-0 baadaye Jumapili.

Goalkeeper Buffon, 39 – ambaye anahitaji mechi 21 kuweka rekodi mpya ya uchezaji mechi nyingi zaidi Serie A, anapanga kustaafu mwisho wa msimu Juve wasiposhinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Previous Post
Kala Jeremiah kumsaka Dr Shika.

Related articles

Simba Yamsajili Adam Salamba.
Roman Abrahamovich ahamia Israel.
Kipa wa Liverpool atishiwa maisha.
Haji Manara, Simba na Yanga…
Serengeti Boys wa Tanzania watwaa…
Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise