
Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya TABORA imepitisha mapendekezo…
Kamati ya Ushauri ya Manispaa ya TABORA imepitisha mapendekezo ya rasimu ya mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2018-2019.
Akiwasilisha mapendekezo hayo katika kikao cha kamati ya ushauri ya manispaa ya TABORA,Mchumi wa Manispaa,JOHANNES KILONZO amesema katika mwaka wa fedha 2018-2019 jumla ya shilingi Bilioni 61 na Milioni 400 zitatumika.
KILONZO amesema mchakato wa maandalizi ya bajeti ya vyanzo vya ndani yamejikita zaidi katika michanganuo ya makisio ya vyanzo mbalimbali.
Kwa upande wake,mkuu wa wilaya ya TABORA,Mwalimu QUEEN MLOZI amewapongeza wajumbe wa kikao hicho kwa kujadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2018-2019.
Amewataka wajumbe wa kikao hicho kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi wanaotumikia na kuachana na masuala yasiyo ya msingi.
Nao viongozi wa siasa,SAIDI LENGWE na ROBERT MHOZYA kwa pamoja wameunga mkono mapendekezo ya bajeti ya bajeti hiyo.’
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Halmashauri ya Manispaa ya TABORA wameutaka uongozi wa Manispaa kuhakikisha makabrasha ya mapendekezo ya bajeti yanawafikia mapema ili waweze kupata muda wa kutosha kuyapitia kabla ya kujayadili.