Kaya 72 katika kijiji cha IMALAKASEKO,kata ya GOWEKO wilayani…
Kaya 72 katika kijiji cha IMALAKASEKO,kata ya GOWEKO wilayani UYUI zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini kwa kuanzisha miradi ya kilimo na ufugaji.
Akitoa taarifa kwa viongozi wa TASAF makao makuu,Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha IMALAKASEKO,LAULENTI KUSAIGWA amesema wananchi waliokuwa wakiwezeshwa na TASAF wamenufaika kwa kiasi kikubwa.
Wakizungumzia jinsi walivyonufaika na mpango wa TASAF wa kunusuru umaskini wanufaika WINFRIDA KATABI,SAID SWEDI na RAMADHAN MUSA wamesema wameanzisha kilimo na ufugaji
Kwa upande wake Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Daktari JASON BAGONZA amesema kuwa lengo la serikali pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini-TASAF ni kusaidia kaya masikini ziondokane na hali ya umaskini na kuishi maisha ya kawaida
Amewataka walengwa wa mpango wa TASAF awamu ya tatu kutumia fedha wanazopewa kwa malengo yaliyokusudiwa na siyo kwa mambo mengine ambayo yanaweza kuendeleza umaskini.