Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

KENYA: Shule yafungwa baada ya tuhuma za kubakwa kwa…

  • June 4, 2018June 4, 2018

Shutuma kali zimeibuka nchini Kenya katika mitandao ya kijamii huku masuali mengi yakiulizwa kuhusu usalama wa watoto wanaosoma katika shule za mabweni baada ya tuhuma kwamba wasichana kadhaa katika shule moja ya upili Nairobi Kenya walibakwa na mtu asiyejulikana ndani ya shule hiyo Jumamosi usiku.

Makundi ya kutetea haki za wanawake yametishia kuandamana leo pamoja na wanafunzi wa zamani wa shule ya upili ya Moi Girls nje ya shule hiyo ya mabweni kwa wasichana kuitaka serikali ichukuwe hatua za kisheria dhidi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Wazazi waliokuwa na ghadhabu waliwasili katika shule ya upili ya Moi mjini Nairobi Jumapili asubuhi kuwachukua watoto wao kufuatia agizo la wizara ya elimu nchini.

Waziri wa elimu Kenya Amina Mohammed amesema watachunguza mapengo yoyote yaliopo na wayashughulikieWaziri wa elimu Kenya Amina Mohammed amesema watachunguza mapengo yoyote yaliopo na wayashughulikie

Akizungumza na waandishi habari alipoizuru shule hiyo, waziri wa elimu nchini Amina Mohammed amesema uchunguzi utaendelea, na kwamba watachunguza mapengo yoyote yaliopo na wayashughulikie.

‘Nataka niwahakikishie kwamba tutaimarisha usalama shuleni, na tutahakikisha kwamba watoto wetu wanapokuja hapa, watasoma kama walivyokuja kusoma’, amesema Waziri Amina.

Kuna mzozo kuhusu idadi kamili ya wasichana wanaotuhumiwa kubakwa, huku ripoti za kukinzana zikitaja mischana mmoja nyingine zikitaja wasichana watatu ndio waliobakwa katika mkasa huo.

View image on Twitter

Gazeti moja nchini linasema msichana mmoja aliyeathiriwa amemtaja mwanamume – aliyemueleza kwa rangi ya ngozi mwilini kuwa ni wa kahawia – aliwashambulia usiku.

Afisa mkuu wa polisi anayelisimamia eneo ambako shule hiyo iko, amethibitisha kuwa msichana wa kidato cha pili alibakwa katika choo kilichoko nje ya bweni, lakini hakuweza kuthibitisha tuhuma kuhusu waathiriwa wengine wawili.

View image on Twitter

NTV Kenya

✔@ntvkenya

Moi Girls School, Nairobi closed after rape incident http://bit.ly/2sDAMvP 

1:02 PM – Jun 3, 2018
  • 6

  • See NTV Kenya’s other Tweets

Twitter Ads info and privacy

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @ntvkenya

Hii sio mara ya kwanza kwa shule hiyo ya Moi Girls kujipata matatani.

Mwaka jana moto wanafunzi 7 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule hiyo.

Idara ya upelelezi nchini sasa inchunguza tuhuma hizo na kwamba maafisa wa shule hiyo waliwataka wanafunzi wanyamaze wasiripoti kisa hicho cha ubakaji.

Baadhi ya wazazi na wakaazi wa eneo la shule hiyo waliojitokeza kujaribu kuwajulia hali wanawao katika shule hiyo baada ya mkasa huo wa moto
Image captionWazazi waliofika katika shule ya upili ya Moi kuwajulia watoto wao baada ya mkasa huo

Kuna tuhuma pia kwamba mwanafunzi huyo wa kidato chapili aliambiwa ajioshe baada ya mkasa huo , na kwamba aliahidiwa kupewa ufadhili wa karo ya shule.

Kwa sasa shule hiyo ya Moi Girls imefungwa kwa angalau wiki moja kuruhusu uchunguzi ufanyike.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Watu 7 wafariki baada ya mlima kulipuka volkano, Guatemala.
Pellegrini aporwa na majambazi wenye bunduki

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise