Kiwango cha ukusanyaji wa damu katika Manispaa ya TABORA…
Kiwango cha ukusanyaji wa damu katika Benki ya Damu Salama Kanda ya Magharibi kimepungua katika Manispaa ya TABORA kutoka lengo la ukusanyaji wa chupa l,709 hadi chupa 828 kwa mwezi Septemba mwaka huu.
Mkuu wa kitengo cha ukusanyaji damu Benki ya Damu,Kanda ya Magharibi, NYAWADE MAGESA amesema baada ya kampeini ya uchangaji damu,wachangiaji wamepungua hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wahitaji.
Ameongeza kuwa kwa sasa kila halmashauri mkoani TABORA inajitegemea katika ukusanyaji wa damu.