Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Korea Kusini yapendekeza mazungumzo ya juu na Kaskazini kuhusu…

  • January 2, 2018

Korea Kusini imetoa ombi la kutaka kufanyika mazungumo ya juu na Korea Kasuni tarehe 9 mwezi huu kujadili ikiwa kuna uwezekano wa kushiriki mashindano ya msimu wa baridi mwaka 2018.

Hii ni baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kusema kuwa alikuwa anatafikiria kutuma timu kwenda Pyeongchang nchini Korea Kusini kwa mashindano hayo mwezi Januari.

Alisema kuwa nchi hizo mbili zinahitaji kukutana kwa dharura kuzungmzia uwezekano wa kushiriki mashindano hayo.

Mapema rais wa Korea Kusini alisema kuwa ameiona hiyo kama fursa ya kuboresha uhusiano ulioharibika kati ya nchi hizo.

Waziri wa mapatano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon alipendekeza Jumanne kuwa wawakilishi watakutana katika kijiji ya mapatano cha Panmunjon.

Kijiji hicho kilicho eneo lenye ulinzi mkali la DMZ mpakani ndipo mazungumzo kati ya nchi hizo yamekuwa yakifanyika.

Bado haujulikani ni nani atahudhuria mazungumzo hayo ya tarehe tisa Januari, na Korea Kaskazinia bado haijajibu.

Mazungumzo ya mwsiho ya juu yalifanyika Disemba mwaka 2015 katika eneo la pamoja la viwanda la Kaesong.

Yalimalizika bila makubaliano yoyote na ajenga ya mazungumzo haikutangazwa.

Chanzo: BBC Swahili.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Spika wa Bunge azungumzia matibabu ya Mh. Tundu Lissu
TCRA yatoa adhabu kali kwa vituo vitano vya Runinga.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise