Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
News

Korea Kusini yasema iko macho kwa kaskazini

  • January 18, 2018

Korea kusini imesema itashughulika na Korea kaskazini kwa kile alichokiita ” Macho ya wazi” baada ya kukamilika mpango wa kuweka timu moja ya pamoja katika michezo ya majira ya baridi ya Olympics inayofanyika mwezi ujao.

Akizungumza na BBC Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea kusini Kang Kyung-wha amesema licha ya makubaliano yaliyopo, dhumuni kubwa linabaki kuwekwa vikwanzo kushughulika na vitisho vya nyuklia.

Amesema mkutano uliojumuisha nchi 20, ambao umefanyika katika mji wa Vancouver ulikuwa ukihusu jinsi bora ya kuweka vikwazo hivyo. Lakini pia amezingatia mahitaji ya kibinadamu kwa watu wa Korea kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea Kusini Kyang Kyung-what ameupongeza ushirikiano huo kati ya nchi yake na kaskazini.

Amesema pia anataka kuona misaada ya kibinadamu ikipelekwa Korea kaskazini.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani Rex Tillerson, amesema nchi yake na washirika wao ikiwemo China, haijawahi wakaunganika pamoja kama sasa dhidi ya kitisho cha nyuklia kilichowekwa na Korea kaskazini.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Hofu baada ya samaki mwenye sumu kali kuuzwa Japan
Mafuriko yazuia wanafunzi kwenda shule.

Related articles

Guardiola alinichukulia kama adui na…
TABORA: Ushiriki wa wazazi kusoma…
Milioni 334 zatengwa kwa ajili…
Macron aanza ziara yake nchini…
Mwakyembe aagiza Nandy akamatwe, Diamond…
Arsenal yanusurika kombe la Yuropa,…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise