Leo ikiwa ni mwaka mpya wa kiislamu,waislamu mkoani TABORA…
Leo ikiwa ni mwaka mpya wa kiislamu,waislamu kote duniani wakikumbuka tukio la Hijra Mtume MUHAMAD kuhama mji mtukufu wa MAKKA kwenda MADINA,waislamu mkoani TABORA wametakiwa kujitathmini na kujikita katika uchamungu.
IMAM wa msikiti mkuu Aljumaa mkoani TABORA Alhaji SHABANI SALUMU SHABANI amewataka waislamu kusherehekea mwaka huu kwa kubadilika kwa kuacha matendo ya kumuasi Allah na kurejea katika misingi ya uislamu.
Amesema miongoni mwa alama za uislamu ni kuupata mwaka mpya hivyo waislamu wanapaswa kumshukuru Allah na kubadilika katika matendo na katika nafsi zao.