Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Leo ni duru ya pili ya uchaguzi wa urais…

  • December 26, 2017

Watu nchini Liberia wanapiga kura katika duru ya pili kati ya makamu wa rais Joseph Boakai na nyota wa zamani wa kandanda Bwana George Weah.

Bwana Weah, 51, alishinda duru ya kwanza lakini hakufanikiwa kupata asilimia 50 ya kura kumwezesha kuwa mshindi.

Duru ya pili ya uchaguzi wa urais kuchukua mahala pake Ellen Johnson Sirleaf, ilichelewa kufuatia kesi iliyokuwa mahakamani.

Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili.

Zaidi ya watu milioni mbili wamejiandikisha kama wapiga kura.

Wagombea ni nani?

Bw. Boakai 73, amekuwa makamu wa rais nchini Liberia kwa miaka 12 lakini haonekani kunufaika na uungwaji mkono kutoka kwa rais.

Naye Weah, ambaye ni nyota wa zamani wa kandanda ana matumaini ya kushinnda baada ya kuwania kwa mara ya tatu.

Alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza mwaka 2005, lakini akashindwa wakati wa duru ya pili.

Wakati wa uchaguzi ulioafuata akiwa mgombea mwenza, muungano wake ulisusia duru ya pili ukidai kuwepo udanganyifu.

Chanzo: BBC Swahili

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Ujerumani yagundua akaunti bandia za Wachina
TABORA: Waganga 86 wanaojihusisha na ramli chonganishi wakamatwa na Jeshi la Polisi

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise