Ligi kuu Tanzania bara kuendelea wikiendi hii huku kukiwa…
Ligi kuu soka Tanzania bara itaendelea kesho na keshokutwa ambapo kutakuwa na michezo saba YOUNG AFRICANS itacheza na NDANDA FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Michezo mingine itakuwa ni Singida United itaialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo utaofanyika Uwanja wa Mwadui ilihali Majimaji itakuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Jumapili Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Mechi zote zitaanza saa 10.00 jioni, Ila mchezo kati ya AZAM na LIPULI utaanza saa 1.00 jioni kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi.