Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Liverpool, Monaco, Spurs zamaliza hatua ya makundi kwa ushindi.

  • December 7, 2017

Michezo nane ya mwisho ya hatua ya makundi ya klabu bingwa barani ulaya imechezwa usiku huu na hivyo kukamilisha jumla ya timu 16 zilizosonga mbele.

Majogoo wa Liverpool, wameibuka na ushindi wa kishindo nyumbani kwa kuichapa Spartak Moscow magoli 7-0 huku Maribor wakitoka sare ya 1-1 na Sevilla hivyo katika kundi E ni Liverpool na Sevilla zinasonga mbele.

Katika kundi F, Waholanzi wa Feyenoord wakaifunga Napoli 2 – 1,nao Shakhtar Donetsk wakapata ushindi muhimu wa mabao 2 – 1 dhidi ya Manchester City hivyo Man City na Shakhtar Donetsk wanasonga mbele katika hatua ya kumi na sita bora.

Wareno wa Fc Porto wakatakata nyumbani kwa ushindi wa goli 5-2 dhidi ya Wafaransa wa Monaco nao Wahuni wa Besiktas wakashinda ugenini kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Leipzig. hivyo katika kundi G,Fc Porto na Besiktas ndio wanafuzu kwa hatua ya kumi na sita bora.

Katika kundi H, Real Madrid na Tottenham zimefuzu kusonga mbele baada ya Real Madrid kuwachapa Borussia Dortmund 3-2, Huku Tottenham Hotspur wakishinda 3 – 0 dhidi ya APOEL Nicosia.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Marekani Kumuonya Odinga.
Serikali imeshauriwa kutekeleza sheria kwa watu wanaofanya vitendo vya ukatili.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise