Maafisa ugani katika wilaya ya IGUNGA mkoani TABORA wametakiwa…

Maafisa ugani katika wilaya ya IGUNGA mkoani TABORA wametakiwa kuwa karibu na wakulima wa zao la pamba ili kanuni,taratibu na sheria za kilimo cha zao hilo zifuatwe.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa TABORA,AGGREY MWANRY wakati akizungumza na wananchi wa kata za ISAKAMALIWA,BUKOKO,MWAMASHIGA, MWAMAKONA, na ITUNDURU wilayani IGUNGA.
Nao baadhi ya maafisa ugani NCHEMBI MPEMBA wa kata ya ISAKAMALIWA na GABRIELI PAUL wa kata ya BUKOKO wamesema watasimamia vyema maelekezo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya IGUNGA,JOHN MWAIPOPO amewataka wananchi kutii sheria ya kilimo bora cha zao la pamba.
Mkuu wa mkoa wa TABORA amehitimisha ziara yake ya siku tano wilayani IGUNGA katika kampeni ya kuongeza tija katika kilimo cha zao la pamba ambapo wananchi pamoja na viongozi wa serikali ya vijiji na kata wamekula kiapo kusimamia vyema kilimo cha zao la pamba.
Asilimia 94 ya zao la pamba katika mkoa wa TABORA huzalishwa katika wilaya ya IGUNGA.